Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Papa atuhumiwa kuwakashifu tena wapenzi wa jinsi moja

Papa Francis Akataa Wanaume Jinsia Moja Kufanya Mafunzo Ya Ukasisi Papa atuhumiwa kuwakashifu tena wapenzi wa jinsi moja

Wed, 12 Jun 2024 Chanzo: Bbc

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameshtumiwa kwa kutumia lugha ya chuki dhidi ya wapenzi wa jinsia moja kwa mara nyengine tena akiwa katika mkutano wa faragha.

Kwa mujibu wa mashirika kadhaa ya habari, inasemekana Papa alitumia neno la dharau kuhusu wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja katika kikao hicho cha faragha katika mji wa Vatican na kusisitiza juu ya tahadhari yake ya kuzuia uwezekano wa wanaume hao kuwa makasisi.

Tuhuma hizi mpya zinaripotiwa ikiwa ni wiki chache toka kiongozi huyo alipolazimika kuomba radhi kwa kutumia neno la kuudhi kuhusu wanaume wapenzi wa jinsia moja. Papa ameripotiwa kutumia neno hilo hilo tena.

Kauli ya awali Papa Francis aliitoa katika mkutano wa faragha na maaskofu mwezi uliopita, alipoelezea vyuo vya ukuhani kuwa tayari vimejaa "frociaggine" - neno la maudhi katika lugha ya kitaliano dhidi ya wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Kulingana na shirika la habari la ANSA, Papa alirudia neno hilo siku ya Jumanne alipokuwa akikutana na mapadre wa Roma, akisema kuna hewa ya "frociaggine" huko Vatican na ni bora vijana wapenzi wa jinsia moja wasiruhusiwe kujiunga na seminari.

Ikijibu tuhuma hizi mpya, Ofisi ya Habari ya Vatikan imekariri taarifa waliyoitoa awali kuhusu mkutano huo wa Jumanne baina ya Papa na Makasisi, ambapo mkuu huyo wa Kanisa Katoliki alikariri hitaji la kuwakaribisha wapenzi wa jinsia moja Kanisani na haja ya tahadhari kuhusu wao kuwa makasisi.

Chanzo: Bbc