Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Papa 'asikitishwa' na uamuzi wa Uturuki kugeuza kanisa kuwa msikiti

Pope Francis Easter Papa 'asikitishwa' na uamuzi wa Uturuki kugeuza kanisa kuwa msikiti

Tue, 14 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amesema kuwa "ameumizwa" na hatua ya Uturuki kugeuza Hekalu la Hagia Sophia mjini Istanbul kuwa msikiti.

Akizungumza katika ibada moja katika makao makuu ya Vatican, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki la Roma aliongeza kuwa mawazo yake "yapo na watu wa Istanbul".

Hagia Sophia ilijengwa kama hekalu la Wakristo karibu miaka 1,500 iliyopita na baadae kugeuzwa kuwa msikiti baada ya mapinduzi ya Ottoman ya mwaka 1453.

Hekalu hilo lililotambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Unesco kama eneo la kihistoria duniani liligeuzwa kuwa makavazi ya kitaifa mwaka 1934 chini ya mwanzilishi wa nchi ya Uturuki padre Ataturk.

Lakini mapema wiki hii mahakama nchini Uturuki iliamuru kuondolewa kwa hadhi ya makavazi katika jengo hilo, ikisema matumizi yake mengine zaidi ya kuwa msikiti "haiwezekani kisheria".

Papa Francis alisema maneno machache kuhusu suala hilo: "Mawazo yangu yawafikie wakaazi wa Istanbul. Nifikiria kuhusu Santa Sophia nahisi uchungu sana."

Rais Recep Tayyip Erdogan amesema ibada ya kwanza ya Kiislamu itafanyika Hagia Sophia Julai 24.

Muda mfupi baada ya tangazo hilo, mwito wa kwanza wa sala au adhana ambayo ilipeperushwa katika vituo vyote vikuu vya habari ilisikika kutoka katika jengo hilo.

Vituo vya mitandao ya kijamii ya Hagia Sophia vimeondolewa mtandaoni.

Makundi yenye itikadi kali ya Kiislam nchini Uturuki kwa muda mrefu yamekuwa yakishinikiza eneo hilo ligeuzwe kuwa msikiti tena lakini wanazuoni na wanachama wa upinzani walipinga hatua hiyo.

Akitetea uamuzi huo, Rais Erdogan alisisitiza kuwa nchi yake imefikia uamuzi wa kitaifa ambao ni haki ya nchi inayojitawala, na kuongeza kuwa jengo hilo litakuwa wazi kwa watu wote- Waislamu, wasiokuwa Waislamu na wageni wa kimataifa.

'Maoni kutotiliwa maanani'

Papa ni mmoja wa viongozi kadhaa wa kidini na kisiasa duniani mbao wamekosoa hatua hiyo.

Baraza la Makanisa Duniani limetoa wito kwa Rais Erdogan kubatilisha uamuzi huo.

Kanisa la Urusi ambalo, lina idadi kubwa ya waumini wa Kikristo wa dhehebu la Orthodox duniani, moja kwa moja lilielezea kusikitishwa kwake na uamuzi uliotolewa a mahakama ya Uturuki likisema kuwa haikutilia maanani maoni yake kabla ya kuamua juu ya kuamua kuhusu kesi ya Hagia Sophia.

Hatua hiyo pia imekosolewa vikali na Ugiriki huku Unesco ikisema Kamati ya Kimataifa kuhusu maeneo ya Kihistoria Duniani huenda ikatathmini upya hadhi ya eneo hilo la kale.

Mmoja wa waandishi maarufu wa Uturuki, Orhan Pamuk, ameiambia BBC kuwa hatua hiyo huenda ikaondoa "fahari" waliokuwa nayo Waturuki dhidi ya nchi hiyo ya Kiislam.

"Kuna mamilioni ya Waturuki kama mimi ambao walipinga hatua hii na ambao sauti zao hazikusikika," alisema Bw. Pamuk.

Historia ya eneo hilo la kihistoria duniani

Historia ya Hagia Sophia ilianza miaka 537 wakati wa utawala wa ukoo wa Justinian ulipojenga built kanisa kubwa ambalo urefu wake uliangalilia chini forodha ya Golden Horn. Kutokana na mnara wake mkubwa, iliaminiwa kuwa kanisa na jengo kubwa zaidi duniani Ilisalia mikononi mwa remained in Byzanite kwa Karne kadhaa isipokuwa mwaka 1204 wakati wanaharakati walipovamia mji huo. Mwaka 1453, katika tukio ambalo lilikua pigo kubwa kwa Wabyzantine, Ottoman Sultan Mehmed II aliteka mji wa Istanbul (uliokuwa ukijulikana kama Constantinople) na kufanikiwa kusali ibada ya Ijumaa katika hekalu la Hagia Sophia Ottomans baadae waligeuza jengo hilo mkuwa msikiti, na kuongeza minara mingine iliyofunika na kubadili muonekano ulioashiria lilikuwa kanisa kwa kuandika maneno ya kiarabu. Baada ya karne kadhaa ya kuwa kati kati ya utawala wa Kiislam wa Ottoman, iligeuzwa kuwa makavazi mwaka 1934 katika juhuza za kuifanya Uturuki kuwa nchi isiyoegemea msingi wa dining moja. Leo hii Hagia Sophia ni eneo maarufu zaidi nchini Uturuki, ambalo linavutia zaidi ya wageni milioni 3.7 kwa mwaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live