Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Papa aridhia Askofu Kilaini kustaafu

Kilainiii 6625 Papa aridhia Askofu Kilaini kustaafu

Sun, 28 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Dunia, Papa Francisco ameridhia ombi la Askofu msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Mkoa wa Kagera, Methodius Kilaini la kustaafu kwake.

Askofu Kilaini aliyetumikia upadri kwa miaka 51 na kuketi nafasi ya uaskofu kwa miaka 24 jana, ombi lake la kutaka kustaafu lilitangazwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga.

Askofu Nyaisonga ametangaza uamuzi huo leo Jumamosi, Januari 27, 2024 ulioridhiwa na Papa Francisco kutoka mjini Roma, wakati ikiendelea misa takatifu kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu Jovitus Mwijage wa Jimbo Katoliki Bukoba

“Tumepata taarifa kutoka Roma muda huu saa nane, ombi la Baba Askofu Kilaini la kutaka kustaafu limekubaliwa rasmi, kwa hiyo amestaafu rasmi tunamtakia kila la kheri,” amesema Askofu Mkuu Nyaisonga.

Baada ya taarifa hiyo, Askofu Kilaini ameitwa sehemu ya kuzungumzia na kuimba, “nimeumaliza mwendo, nimeumaliza mwendo, nimevipiga vita vilivyo vizuri…” huku wakiitikia wimbo huo. Ni wimbo unaotoka 2 Timothea 4;7.

Kisha Askofu Kilaini mwenye miaka 85 akasema, alimualika Rais mstaafu Jakaya Kikwete katika shughuli hiyo lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake ameshindwa kufika, hivyo Kikwete alimwandikia ujumbe mfupi wa kushikwa kwake kufika ambao Kilaini aliusoma.

“Viongozi wa kiroho waendelee kuiombea Tanzania, ninaomba muendelee kushirikiana na Serikali ya awamu ya sita kuhimiza Watanzania tunu za umoja, amani na mshikamano bila kujadli utofauti wa dini rangi na siasa,” aliandika Rais Kikwete.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Kanisa Katoliki Tanzania (Wawata), Eveline Ntenga amesema Askofu Kilaini alikuwa ‘Encycopia’ ndani ya kanisa.

“Alitufunza mengi, aliijua Wawata kuliko tunavyoijua, hakika tulimfaidi ndani ya kanisa, anafahamu mambo mengi ninachomuomba asituchoke tutaendelea kujifunza kutoka kwake kama baba kwa kuwa utumishi wa kanisa haukomi,” amesema.

Askofu Kilaini aliyezaliwa Machi 30, 1938 katika Kijiji cha Katoma, Bukoba Tanzania, baada ya majiundo yake ya awali (maandalizi ya kuwa padri), shule ya msingi, sekondari na mafunzo ya seminari ndogo na Kuu.

Askofu huyo alipewa daraja la padri wa Jimbo la Bukoba akiwa jijini Roma masomoni mnamo Machi 18, 1972 katika mikono ya Kardinali Agnelo Rossi baada ya kupata shahada ya pili ya taalimungu, Roma.

Askofu Kilaini baada ya kurudi Tanzania akiwa padri alifanya kushughuli za kichungaji parokiani, baadaye alikuwa mhazini msaidizi wa jimbo katoliki la Bukoba.

Kati ya mwaka 1978 hadi 1985 alifundisha Historia ya Kanisa katika Seminari Kuu ya Ntungamo na mwaka 1985 na alirudi mjini Roma kuendelea na masomo na kupata shahada ya udaktari wa tauhidi katika historia ya kanisa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana 1990.

Kwa mara nyingine mwaka 1990 hadi 2000 alikuwa katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na   Desemba 22, 1999 aliteuliwa  kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam na kupewa wakfu wa kiaskofu Machi18, 2000 jijini Dar es Salaam.

Desemba 3, 2009 hayati Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI alimteua kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live