Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Papa aiona amani mkutano wa Trump, Kim

65078 Pic+papa

Tue, 2 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Vatican City. Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis ameupongeza mkutano kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un kwa kusema anatumaini kuwa utatoa mwelekeo wa amani.

Akizungumza na maelfu ya watu katika ibada ya baraka ya kila juma kwenye uwanja wa ibada wa Mtakatifu Petro, amenukuliwa akisema kwamba saa chache zilizopita kumeshuhudiwa mfano mzuri wa mkutano usio wa kutarajiwa.

Anawapa wahusika salamu ya sala kwa kuwa ishara hiyo muhimu inaonesha kupigwa kwa hatua, si tu kwenye eneo hilo la rasi bali ni hatua njema kwa ulimwengu mzima.

Trump amekuwa rais wa kwanza wa Marekani akiwa madarakani kuikanyaga ardhi ya Korea Kaskazini, pale alipokutana na kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un, katika eneo lisilo la kijeshi (DMZ) linalozikutanisha Korea Kaskazini na Kusini ambapo pande zote zimekubaliana kuanzisha upya mazungumzo ya nyuklia yaliokwama.

Chanzo: mwananchi.co.tz