Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Papa achapisha waraka mpya "sote ni ndugu tushughulikie matatizo"

FLQXF7AURVGLPJYOZBXV2JZHEU 660x400 Papa achapisha waraka mpya "sote ni ndugu tushughulikie matatizo"

Tue, 6 Oct 2020 Chanzo: millardayo.com

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amechapisha Waraka mpya wa Kitume, akitoa wito wa kuwepo mshikamano katika jamii ili kuweza kuyashughulikia matatizo ya ulimwengu.

Katika waraka huo wa Kipapa uliopewa jina ”Fratelli Tutti”, yaani ”Sote ni Ndugu,” na kutolewa jana katika Uwanja wa Mtakatifu Peter, Vatican City umezikosoa sera za kinadharia kuhusu soko la kibepari kama suluhisho pekee la matatizo ya dunia.

Papa Francis amegusia matatizo ya dunia kama vile mabadiliko ya tabia nchi, dhuluma zinazosababishwa na ukosefu wa usawa wa kiuchumi, tatizo la wahamiaji na janga la virusi vya corona.

Waraka wa Kitume ni moja ya njia ya mawasiliano muhimu ya Papa na hutumika kama msingi wa mafundisho ya Kanisa Katoliki kwa kuangazia msimamo kuhusu masuala muhimu.

TAZAMA BALOZI AVUA BARAKOA MBELE RAIS MAGUFULI, AMPONGEZA JPM IKULU

Chanzo: millardayo.com