Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Papa Fransisko aipandisha hadhi Jimbo Katoliki Mbeya

32781 Pic+katoiki Tanzania Web Photo

Fri, 21 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baba Mtakatifu, Fransisko amemteua Mhashamu Askofu Gervas Nyaisonga kuwa Askofu Mkuu wa kwanza wa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya baada ya kanisa hilo kulipandisha hadhi Jimbo Katoliki la Mbeya.

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Desemba 21, 2018 na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Charles Kitima amesema Askofu Nyaisong alikuwa Askofu wa Jimbo la Mpanda kabla ya uteuzi wake.

Kitima amesema Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya litajumuisha majimbo ya Iringa na Sumbawanga.

Jimbo la Mbeya lilikuwa likiongozwa na Askofu Evaristo Chengula ambaye alifariki dunia Novemba 21, 2018 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.



Chanzo: mwananchi.co.tz