Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Papa Francis kuzuru maskini wa Afrika kuanzia Jumatano

73921 Papapic

Mon, 2 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Vatican City, Holy See. Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis keshokutwa Jumatano anaanza ziara ya wiki moja, akitembelea nchi za Afrika ambazo zimekumbwa na umaskini, vita na majanga ya asili.

Papa Francis atatembelea Msumbiji, Madagascar pamoja na Mauritius, nchi ambazo zilitembelewa na papa John Paul II mwaka 1988 na 1999.

Wachambuzi wanaona uamuzi huo wa papa kutembelea nchi mbili kati ya nchini maskini kuliko zote duniani, kuwa ni kitendo cha mshikamano kutoka kwa kiongozi ambaye mara kwa mara amekuwa kwenye vitongoji maskini nchini Argentina.

Msumbiji ni ya kwanza katika ziara yake, na ujumbe wa papa uliorekodiwa kwa lugha ya Kireno kabla ya ziara yake , unataja ziara ya Papa John Paul.

Lakini mtu anayejulikana kama "papa wa maskini" ataweza kutembelea miji mitatu tu mikuu ya nchi hizo.

Uamuzi huo hautawafurahisha wananchi wa jiji la Beira ambao uko katikati ya Msumbiji, ambako kimbunga kinachoitwa Idai kiliua watu wasiopungua 600 na kuacha maelfu wakiwa hawana makazi mwezi Machi.

Pia Soma

Advertisement   ?
Miezi sita baadaye, watu wengi bado hawana makazi na wanakosa chakula cha uhakika.

"Nilikuwa nategemea papa atakuja kukanyaga ardhi ya Beira," alisema msichana mwenye umri wa miaka 45, Maria da Paz alipoongea na AFP, huku akijifariji kutokana na ukweli kuwa baadhi watakuwa jijini Maputo kukutana na kiongozi huyo wa kidini.

Papa Francis, katika video yake ya ujumbe huo, alitegemea kuwepo na watu ambao wasingefurahishwa na kutotembelewa.

"Ingawa sitaweza kutoka nje ya makao makuu, moyo wangu unawafikia nyingi wote, ukiwa na nafasi9 maalum kwa wale wanaoishi katika mazingira madumu," amesema, akiongeza: "Wote nawakumbuka kwenye sala zangu."

'Papa anatakiwa kuleta matumaini'

Serikali ya Msumbiji imetumia dola 330,000 za Kimarekani (sawa na zaidi ya Sh650 milioni za Kitanzania) kwa ajiloi ya ziara ya papa, kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje, Jose Pacheco, ikiwa ni pamoja na kufanyia ukarabati kanisa kuu la Maputo na kuboresha barabara za jiji hilo.

Ziara ya Papa Francis inakuja mwezi mmoja baada ya serikali kusaini mkataba wa kihistoria wa amani na waasi wa zamani, Renamo, ambao sasa ndio chama kikuu cha upinzani.

Vita ya miaka 16 ya wenyewe kwa wenyewe uliiharibu nchi, na Renamo haijatua silaha kikamilifu.

Katika video yake, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki amesisitiza haja ya kumaliza tofauti nchini Msumbiji na Afrika yote, "kitu ambacho ni tumaini pekee la amani imara na ya kudumu".

Chanzo: mwananchi.co.tz