Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Papa Francis kuachia ngazi

Papa Francis 22.jpeg Papa Francis kuachia ngazi

Mon, 1 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis (85) amesema kuwa safari yake ya hivi karibuni ya Canada imemuonyesha ya kuwa anaweza akahitaji kuachia ngazi.

Kiongozi huyo amesema kutokana na umri na matatizo ya kutembea hatoweza tena kusafiri safari za mbali na safari hii ilikuwa kama "mtihani" kwake.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa safarini kutokea Canada kiongozi huyo ameeleza kuwa "sikuwahi kufikiria kujiuzulu lakini mlango upo wazi, na hakuna tatizo lolote Papa akijiuzulu , sio ajabu na si janga, kubadili papa kunawezekana."

Hii si mara ya kwanza kwa papa Francis kusema kuwa kama afya yake ikimlazimu anaweza kufuata nyayo za mtangulizi wake Benedict XVI aliyeweka historia na kujiuzulu mwaka 2013 kutokana na kudhoofika kwa afya yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live