Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Papa Francis awasili Msumbuji

74239 Papa+pic

Thu, 5 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Maputo, Msumbiji. Kiongozi wa Kanisa Katoliki dunia, Papa Francis amewasili nchini Msumbiji kwa ziara ya kihistoria barani Afrika.

Kiongozi huyo anatarajiwa kufanya ziara ya wiki moja kutembelea nchi za Afrika ambazo zimekumbwa na umaskini, vita na majanga ya asili zikiwamo Madagascar, Mauritius na Msumbiji ambazo zilitembelewa na papa John Paul II mwaka 1988 na 1999

Katika siku ya kwanza ya ziara yake nchini Msumbiji, Papa Francis anatajaa kuzungumzia mambo mbalimbali ikiwamo tatizo la umaskini katika nchi za Afrika, uhifadhi wa mazingira na ufisadi.

Wahudumu katika Kanisa Katoliki wamenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari wakisema kwamba ziara hii ambayo ni ya pili Papa Francis kuwahi kuifanya Kusini mwa jangwa la Sahara, ni fursa muhimu kutoa wito mpya uliogubikwa katika barua yake ya 2015 "Laudato Si" inayuhusu kulinda mazingira.

Kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia (WB), Msumbiji imepoteza hekari milioni nane za misitu katika miaka ya 70 kutokana na mmomonyoko wa udongo na kuchangia nchi hiyo kuwa katika hatari ya kupatwa na vimbunga.

Wachambuzi wanaona uamuzi huo wa papa kutembelea nchi mbili kati ya nchini maskini kuliko zote duniani, kuwa ni kitendo cha mshikamano kutoka kwa kiongozi ambaye mara kwa mara amekuwa kwenye vitongoji maskini nchini Argentina.

Pia Soma

Advertisement
Msumbiji ni ya kwanza katika ziara yake, na ujumbe wa papa uliorekodiwa kwa lugha ya Kireno kabla ya ziara yake , unataja ziara ya Papa John Paul.

Lakini mtu anayejulikana kama "papa wa maskini" ataweza kutembelea miji mitatu tu mikuu ya nchi hizo.

Uamuzi huo hautawafurahisha wananchi wa jiji la Beira ambao uko katikati ya Msumbiji, ambako kimbunga kinachoitwa Idai kiliua watu wasiopungua 600 na kuacha maelfu wakiwa hawana makazi mwezi Machi.

Miezi sita baadaye, watu wengi bado hawana makazi na wanakosa chakula cha uhakika.

"Nilikuwa nategemea papa atakuja kukanyaga ardhi ya Beira," alisema msichana mwenye umri wa miaka 45, Maria da Paz alipoongea na AFP, huku akijifariji kutokana na ukweli kuwa baadhi watakuwa jijini Maputo kukutana na kiongozi huyo wa kidini.

Papa Francis, katika video yake ya ujumbe huo, alitegemea kuwepo na watu ambao wasingefurahishwa na kutotembelewa.

"Ingawa sitaweza kutoka nje ya makao makuu, moyo wangu unawafikia nyingi wote, ukiwa na nafasi9 maalum kwa wale wanaoishi katika mazingira madumu," amesema, akiongeza: "Wote nawakumbuka kwenye sala zangu."

 

Chanzo: mwananchi.co.tz