Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Papa Francis atangaza Mafinga kuwa jimbo jipya

Papa Francis Ataka Kuzikwa Nje Ya Vatican Papa Francis

Mon, 25 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Fransisko ametangaza eneo la Mafinga mkoani Iringa kuwa Jimbo Jipya Katoliki na kumteua Padri Vincent Mwagala wa Jimbo Katoliki la Iringa kuwa askofu wa kwanza wa jimbo hilo jipya.

Kwa mujibu wa taarifa ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) iliyosainiwa na katibu wake mkuu, Padri Charles Kitima, Desemba 22, 2023,

uteuzi huo unaanza leo huku jimbo hilo likipewa jina katika lugha ya kilatini ‘Mafingens’. Askofu Mteule Mwagala amezaliwa Desemba 11, 1973 huko Makungu Wilaya ya Mufindi,

Jimbo Katoliki la Iringa. Baada ya masomo ya upadri, alipewa daraja takatifu la upadri Julai 11, 2007 jimboni Iringa na kuhudumu katika nafasi tofauti za utume nchini Italia na jimboni Iringa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live