Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Papa Francis ataka muafaka Sudan

61983 Pic+papa

Mon, 10 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Katika hotuba yake ya kila wiki alitoitoa jana June 9, katika Uwanja wa Mtakatifu Petero, kiongozi huyo amesema kuwa habari kutoka Sudan zinatia uchungu na wasiwasi.

Kiongozi huyo alisema analiombea taifa hilo ili ghasia zisitishwe na kufikia maelewano kupitia mashauriano.

Kauli ya Papa Francis inafuatia zaidi ya watu 100 kufariki dunia wiki iliyopita baada ya jeshi la nchi hiyo kutumia risasi za moto kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakiandamana katikati ya jiji la Khartoum wakishinikiza kuwapo kwa utawala wa kiraia.

Mapema wiki hii jeshi la Sudan liliwakamata viongozi watatu wa upinzani ikiwa ni siku moja baada ya mazungumzo ya usuluhishi yaliyofanywa na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Dk Abily Ahamed.

Kufuatia hali hiyo taasisi ya wana taaluma nchi humo jana ilitangaza kampeni ya uasi wa kiraia nchi nzima hadi pale jeshi litakapokabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia.

Chanzo: mwananchi.co.tz