Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Papa Francis aomba Serikali zisitishe usafirishaji haramu wa binadamu

Papa Francis Aomba Serikali Zisitishe Usafirishaji Haramu Wa Binadamu Papa Francis aomba Serikali zisitishe usafirishaji haramu wa binadamu

Mon, 6 Mar 2023 Chanzo: Voa

Mkuu wa kanisa katoliki ulimwenguni Papa Francis Jumapili ameomba serikali zisitishe usafirishaji haramu wa binadamu kweye bahari ya Mediterranean.

Hayo amesema wakati akieleza huzuni yake kutokana na ajali ya boti ya wiki iliyopita karibu na ufukwe wa Italy wa Calabrian, ambapo darzeni ya watu walikufa. Wakati akitoa hotuba yake kwenye bustani za St Peter’s mjini Vatican, Papa Francis alisema kwamba,” Natoa wito wangu tena wa kuzuiliwa kwa matukio kama hayo .

Tunaomba walanguzi haramu wa binadamu wakomeshwe.” Mamlaka za kieneo zimesema kwamba kufikia sasa, miili 70 imepatikana kufutia ajali hiyo. Wahamijai waliokuwa kwenye boti iliyopata ajali wanasemekana kutokea Uturuki wengi wakiwa ni raia wa Afghanistan, Pakistan, Iran, Somalia na Syria.

Takriban watu 80 walinusurika kwenye ajali hiyo karibu na mgahawa wa kitalii wa Steccato di Cutro, karibu na ufukwe kwa Calabria mashariki mwa Italy. Boti hiyo inakisiwa kubeba watu 200 kabla ya ajali hiyo kutokea.

Chanzo: Voa