Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Papa Francis akwama kwenye lifti, awaomba radhi waumini

73816 Papa+pic

Mon, 2 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Vatcan City. Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis ameomba radhi kwa kuchelewa misa katika kanisa la Mt. Petro na kusema alikwama kwenye lifti akiwa anakwenda kanisani.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la BBC, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 82 alikwama kwenye lifti kwa dakia 25 leo Jumapili Septemba 1, 2019 mara baada ya umeme kukatika na kuweza kutoka kabla ya kikosi cha wazima moto hakijawasili.

“Ninapaswa kuomba radhi kwa kuchelewa,” Papa Francis aliwaeleza waumini wake huku akitabasamu na kuwataka waumini wote kuwapongeza zimamoto kwa kazi kubwa waliyofanya.

Papa akiwahutubia umati wa watu kusema “kumekuwa na hitilafu ya umeme hivyo lifti ilisimama. Namshukuru Mungu na kikosi cha zimamoto kwa kufika kwa wakati.”

Televisheni moja iliyokuwa ikirusha matangazo ya moja kwa moja ya sala hiyo walihisi Papa huyo amechelewa kufika katika misa kutokana na sababu za kiafya, shirika la habari la AFP limeripoti.

Wakati huohuo, Papa huyo alitangaza pia kuwa mwezi ujao, atatangaza makadinali 10 wapya wa kanisa katoliki.

Pia Soma

Advertisement   ?
 

Chanzo: mwananchi.co.tz