Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Padri agongwa, akutwa na sadaka za wizi kwenye gari

Wed, 24 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Los Angeles, Marekani AFP. Wafanyakazi wa kitengo cha dharura walioenda kutoa huduma katika gari iliyopata ajali mjini California mwezi uliopita, walikuta kasisi akiwa amevunjika mfupa wa pajani, na kilichowashangaza zaidi, ni begi la fedha taslimu zinazodaiwa kuibwa kanisani.

Dayosisi ya Santa Rosa, kaskazini mwa San Francisco, ilisema katika taarifa yake uzi kuwa dola 18,000 za Kimarekani (sawa na zaidi ya Sh40 milioni za Kitanzania) ambazo zilikuwa sadaka za kanisani, zilikutwa kwenye gari la father Oscar Diaz wakati wa ajali hiyo iliyotokea Juni 17.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa uchunguzi zaidi ulibaini "wizi wa muda mrefu," huku zaidi ya dola 95,000 za Kimarekani (sawa na takriban Sh200 milioni za Kitanzania) zilitoweka katika parishi ambazo Diaz, mwenye umri wa miaka 56, alitumikia katika kipindi cha miaka 15.

"Nimechukizwa sana kwamba hili limetokea na nimesikitishwa sana kwmba parishi alizokuwa akihudumia zimeathirika," alisema Askofu Robert Vasa katika taarifa yake.

"Kiwango kamili cha wizi hakijajulikana na kinaweza kisijulikane kabisa katika kila usharika aliotumikia."

Vasa alisema Diaz, ambaye amekuwa kasisi kwa miaka 25, aliwaambia maofisa wa kitengo cha dharura kuwa fedha hizo kwenye mabegi zilikuwa ni mishahara yake.

Lakini wafanyakazi wa hospitalini walikuwa na wasiwasi na kiwango cha fedha ambacho Diaz alipeleka kwenye chumba cha dharura na wakawasiliana na polisi, ambao waliitaarifu dayosisi.

Vasa alisema upekuzi katika ofisi ya Diaz na sehemu ambayo alikuwa akiishi, ulibaini mifuko miikubwa ya makusanyo iliyokuwa na fedha taslimu. Uchunguzi zaidi pia ulionyesha Diaz aliweka fedha katika akaunti yake binafsi benki akitumia hundi ambazo ziloitoka katika sharika hizo.

Vasa alisema Diaz alikiri kuwa alikuwa akiiba mifuko ya kukusanyia fedha makanisani kwa muda mrefu.

"Kwa sasa Father Oscar amesimamishwa kutoa huduma za kiunjilisti," alisema. "Hakuna mipango ya uinjiliti kwa sasa kanisani na hali yake ya baadaye haijulikani."

Lakini alisema dayosisi yake haina mpango wa kumfungulia mashtaka kwa sasa kutokana na gharama.

Chanzo: mwananchi.co.tz