Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Padri Mwekibindu afariki dunia

Mon, 14 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Paroko wa Parokia ya Mikocheni, Padri Andrew Mwekibindu amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Taarifa iliyotolewa na katibu wa Jimbo Kuu Dar es Salaam, Padri Frank Mtavangu imesema, Mwekibindu alifariki usiku wa kuamkia leo Jumapili Januari 13, 2019.

“Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwandama Polycarp Kadinali Pengo anasikitika kutangaza kifo cha Padri Mwekibindu, taratibu za mazishi zinapangwa. Tumuombee pumziko la milele mbinguni. Amina,” ilieleza taarifa hiyo ya Mtavangu.



Chanzo: mwananchi.co.tz