Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Padri Filbert Mhasi ateuliwa kuwa Askofu Jimbo la Tunduru

30777 Padri+pic TanzaniaWeb

Mon, 10 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amemteua Padri Filbert Mhasi kuwa Askofu wa Jimbo la Tunduru-Masasi.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima imeeleza kuwa, kabla ya uteuzi huo Padri Mhasi alikuwa Paroko katika Jimbo la Mahenge mkoani Morogoro.

 “Mwaka 2014 mpaka sasa alikabidhiwa majukumu ya uparoko katika kanisa kuu la Jimbo la Mahenge,” imesema taarifa hiyo.

Mhasi alizaliwa Novemba 30, 1970 na kwa vipindi tofauti  amekuwa akitoa huduma mbalimbali kwenye kanisa hilo tangu alipokuwa Padri Julai 3, 2001.

Alipata   elimu   ya   falsafa   katika seminari kuu ya Kibosho (1993-1995) na elimu ya teolojia   katika   seminari   ya   Mtakatifu Paulo,  Kipalapala   (1995-1998).

Ametoa   huduma   sehemu   mbalimbali   ndani   ya   Jimbo   la Mahenge, msaidizi wa Gombera seminari ya Kasita (2003-2004),   Gombera   wa   seminari   hiyo   (2009-2014).

 

 

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz