Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ofisi ya Mufti Z’bar yamruka Shehe Ponda

Muft Ofisi ya Mufti Z’bar yamruka Shehe Ponda

Thu, 22 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

VIONGOZI wa dini wametakiwa kutochanganya siasa na imani za dini, jambo ambalo linaweza kusababisha uvunjifu wa amani na utulivu kuelekea uchaguzi mkuu wa wiki ijayo.

Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Shehe Khalid Ali Mfaume alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana na kukanusha msimamo uliotolewa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Shura ya Maimamu Shehe Issa Ponda, kwamba Waislamu nchini wamekubaliana kumpa kura za ndiyo mgombea wa Chama Cha Demokrasia (Chadema), Tundu Lissu katika uchaguzi mkuu wa wiki ijayo.

Alisisitiza kuwa hakuna makubaliano ya aina hiyo kati ya Waislamu nchini na taasisi hiyo ya Shura ya Maimamu nchini katika mtazamo wenye msimamo wa kisiasa katika uchaguzi mkuu.

Alisema kila raia wa Tanzania, anao uhuru wa kuchagua kiongozi anayemtaka kwa mujibu wa katiba;na suala la imani ya dini ni uamuzi wa mtu binafsi.

“Ofisi ya Mufti wa Zanzibar inatoa taarifa ya kukanusha kuhusu tamko lililotolewa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Shura ya Maimamu kwamba Waislamu wamefikia makubaliano ya kumpigia kura za ndiyo katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lissu” alisema.

Shehe Mfaume aliwaeleza wananchi na Waislamu kuwa wanatakiwa kufahamu msemaji mkuu wa jamii ya Waislamu kwa upande wa Zanzibar ni Mufti wa Zanzibar, Shehe Saleh Kabi.

Alisema Msemaji Mkuu kwa Waislamu kwa upande wa Tanzania Bara ni Mufti Shehe Abubakary Zubeir, ambaye pia anatambuliwa na taasisi na jumuiya mbalimbali za Waislamu.

''Hao ndiyo wasemaji wakuu wa jamii ya Waislamu kwa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara...Shehe Ponda sisi hatumfahamu na Waislamu wote wanatakiwa wampuuze''alisema.

Chanzo: habarileo.co.tz