Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngoma nzito! Wazee wawaangukia waumini sakaka la kuondolewa Mch. Kimaro

Mch. Kimaro Asd Wazee wawaangukia waumini sakaka la kuondolewa Mch. Kimaro

Thu, 19 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sakata la Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kijitonyama, Dk. Eliona Kimaro, limezidi kushika kasi huku waumini wa usharika huo wakizidi kuweka shinikizo la kutaka arejeshwe na kuendelea na huduma.

Dk. Kimaro alipewa likizo ya siku 60 na uongozi wa juu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP) na kwamba baada ya likizo hiyo, anatakiwa kuripoti makao makuu ya Dayosisi, Luther House, jijini Dar es Salaam.

Jana asubuhi, ikiwa ni siku moja baada ya waumini kukusanyika eneo la kanisa wakiwa na mabango, katika ibada, idadi ya waumini ilikuwa ya kuhesabu tofauti na ilivyozoeleka, huku baadhi ya waumini waliokuwa nje ya kanisa wakionyesha ishara ya kudai kurejeshwa kwa mchungaji wao.

Jana waumini walioruhusiwa kushiriki ibada hiyo ni wale ambao uongozi wa usharika uliwahoji taarifa zao mlangoni kujua kama ni washirika. Baada  ya ibada hiyo, Mzee wa Kanisa alitoa tangazo ibadani hapo kusema wanaungana na waumini wengine kuombea tukio la kusimamishwa kwa Mchungaji Kimaro.

Alisema baraza la wazee la usharika linashughulikia suala hilo kwa kushirikiana na mamlaka zingine zinazohusika na kuwasihi wawe watulivu kwa kuishi katika sala na toba.

“Mtu awaye yote asizuie masifu ya asubuhi wala masifu ya jioni wala ibada yoyote kwa sababu Mungu wetu ni wa utaratibu naye ametuwekea utaratibu. Msije mkadhani kwamba jambo hili halishughulikiwi. Wazee wenu wanalishughulikia kwa kushirikiana na mamlaka zote kuweka sawa,” alisema.

Alisema wale waliochapisha fulana na ujumbe wa kwenye mabango zitumike kuingia kanisani ambako ni sehemu sahihi ya kuzungumzia na kuombea mambo yote badala ya nje ya kanisa.

“Mtu ana suala lake kuhusu suala hili, wote tukutane ndani ya nyumba ya ibada kwa ajili ya kuliombea ndipo Mungu atatujibu katika hema ya kukutania na wala usiandamane tukutane hapa, humu ndani ndio inaleta amani,” alisema.

Alifafanua kuwa, yeyote atakayefanya kinyume na walioyaelekeza watamhesabia mtu kama anataka kutuletea fujo ambazo hatuzitaki na si utamaduni wao.

“Tuwe na utulivu na tuwe na subira. Katika  kila jambo Mungu ana kusudi lake, hivyo tumpe Mungu nafasi, atatenda kwa wakati wake, niwashukuru wote mlioshukuru ibada ya asubuhi na wale mtakao kuja ile ya jioni.

“Wapo wanaotutakia mema na wasiyotutakia mema yamkini nyie wacha Mungu mtakuwa na utulivu huo lakini watakuwapo wengine ambao watatumia fursa hii kufanya mambo ambayo siyo wasilichafue kanisa wasituchafue kwa maana lipo imara, tunaomba utulivu,” alisisitiza.

MSIMAMO WA WAUMINI

Licha ya taarifa iliyotolewa na uongozi wa baraza la wazee, waumini wanaopinga kuondolewa kwa Dk. Kimaro, waliendelea kuhimiza kukutana madhabahuni kwa ajili ya kupaza sauti zao kushinikiza arudishwe.

Katika mitandao ya kijamii yakiwamo makundi ya Whatsapp, waumini waliendelea kuhimiza kutonyamaza hadi suala hilo litakapotafutiwa ufumbuzi.

ASKOFU SHOO ATIA NENO

Akizungumza na moja ya chombo cha habari juzi Mkuu wa KKKT, Dk. Fredrick Shoo, aliwaomba utulivu kwa washarika na wakristo ambao wamesikia habari za uamuzi uliofikiwa na dayosisi yake.

"Tutambue kuwa dayosisi ina vyombo vyake vya maamuzi na bila shaka jambo lenyewe linaendelea kufanyiwa kazi na dayosisi husika, baadaye sisi ambao tumepokea taarifa kama hizi tunaendelea kufuatilia na kupata taarifa zaidi kuhusu jambo hili ambalo linaonyesha limeleta usumbufu na mwitikio tofauti kutoka kwa watu wengi.

"Kubwa sana ambalo ningeomba wakristo hawa waumini wa usharika wake waweze kuwa watulivu wakati jambo hili linaendelea kufanyiwa kazi," alisisitiza Askofu Shoo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live