Dar es Salaam. Kiongozi wa kanisa la Inuka Uangaze, Nabii na mtume Boniface Mwamposa amelazimika kusitisha ibada kwa ajili ya kuitikia wito wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Tanzania kulikotokea vifo vya waamini wake.
Mwamposa ambaye huendesha ibada zake katika eneo la Tanganyika Packers, leo Jumapili Februari 2, 2020, amelazimika kufupisha ibada ya kwanza na kuanza safari ya kuelekea Moshi alikoitwa na polisi.
Kawaida ibada hiyo huisha kati ya saa saba hadi saa nane mchana, lakini leo imeisha saa 4:30.
Mwamposa akiwa ameambatana na wasaidizi wake, aliondoka katika eneo hilo la Kanisa 4:30 asubuhi hii.
Jana katika kongamano lake la kukanyaga mafuta ya upako mkoani Kilimanjaro, watu 20 walipoteza maisha wakisukumana kukanyaga mafuta hayo.
Wakati hayo yakiendelea, waumini wa nabii huyo wamemkingia kifua na kueleza suala la watu kukanyagana kwenye mikutano mikubwa ni kawaida.
Habari zinazohusiana na hii
- VIDEO: 20 wafariki wakigombea kupaka mafuta ya upako mjini Moshi
- VIDEO: Majeruhi asimulia tukio zima la Mchungaji Mwamposa kumwaga mafuta ya upako
- VIDEO: Polisi Tanzania wamtaka Mtume Mwamposa kujisalimisha