Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabii Bruno: Sherehekeeni mkiliombea Taifa

Maombezi Iringa.jpeg Mmoja wa waumini wa kanisa la PBIM, Manispaa ya Iringa akiombea Taifa la Tanzania

Sun, 25 Dec 2022 Chanzo: Mwananchi

Watanzania wametakiwa kuliombea Taifa ili amai iliyopo iendelee kudumu.

Akizungumza wakati wa mkesha wa Chrisimasi ulioambatana na maombi ya kuliombea Taifa la Tanzania, Nabii wa kanisa la PBIM, Manispaa ya Iringa Nabii Bruno Massae alisema kila mwenye imani hana budi kufanya hivyo.

Alisema majanga mbalimbali kama ukame, ajali za barabarani, matukio ya kikatili hasa kwa watoto na wanawake yanaweza kumalizika kukiwa na watu wanao liombea Taifa.

"Waombee viongozi wote kuanzia Rais, mawaziri, wabunge ili wanapotoa maamuzi ya nchi watoe kulingana na Mungu anavyotaka Taifa letu liwe," alisema Nabii Bruno.

Alisema sikukuu ya Krismasi sio tu kula na kunywa isipokuwa kutafakari kazi ambazo Yesu alifanya kubwa ikiwa ni upendo.

"Hata kama ungetoa sadaka mamilioni kwa mamiliona kama huna upendo ni kazi bure, Christmas ni upendo wa Mungu kwetu sisi wanadamu," alisisitiza.

Kwa upande wake Mchungaji Andrew Kiwele, alisema suala la kuombea Taifa ni la kila mmoja.

"Ukiamka ombea nchi yako, ukilala ombea nchi yako hii ndiyo Mungu amekupa, tusione uzito, tuwe wazalendo na tuisemee nchi yetu yaliyo mema," alisema Kuwele.

Chanzo: Mwananchi