Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee wa Upako: Nina magari ya kifari hatari

MZEE WA UPAKO MAGARI YA KIFAHARI Mzee wa Upako: Nina magari ya kifari hatari

Mon, 3 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchungaji Anthony Lusekelo (Mzee wa Upako) amewataka watumishi wa Mungu Mitume na Manabii kuacha kuwa na tamaa ya mali na wajikite kwenye utumishi wa Mungu huku akitolea mfano maisha yake ya kifahari lakini hajamuacha Mungu.

Amedai anamiliki magari yakifahari kama Nissan ya Tsh Mil 400, gari aina ya Cadillac ambayo hajaitumia kwa miaka 7 lakini moyoni kwake kinachompa nguvu ni Mungu ambaye amekuwa akimuabudu.

“Nissan ya Tsh Mil. 400, Cadillac, nyie mnatembelea vimeo,” alisema.

Ameyasema hayo Jumamosi iliyopita katika Mkutano wa Mitume na Manabii ambao umefanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar Es Salaam na kuhudhuriwa na watumishi wa Mungu kutoka katika mikoa mbalimbali.

Mkutano huo ulikuwa na lengo lakukumbushana baadhi ya vitu ambavyo vimekuwa vikifanya waache maswali mengi kwa jamii kuhusu mienendo yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live