Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee aliyehudumu Ukuu wa Mkoa ndani ya mikoa 7 atapeliwa nyumba na Wachina (Video)

Sat, 3 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Mzee Juma Waziri (90) ambaye amedai alihudumu nafasi ya Ukuu wa Mkoa ndani ya Mikoa 7, amedhulumiwa nyumba na Wachina ambao amedai ni wapangaji wake kwa miaka 20.



Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa hii, Mzee Waziri alidai alishangaa nyumba yake hiyo ikipigwa mnada ya benki na baadaye mpangaji wake huyo kuinunua nyumba hiyo.

“Kusema kweli hatujui nani alikopa huo mkopo ambao umesababishwa nyumba kuuzwa, hata benki wamekataa kutueleza wanataja jina na mtu anaitwa Mwana Mipango, sisi hatumjui,” alisema Mzee huyo kwa uchungu.

Mzee huyo amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kuingilia sakata hilo na kuhakikisha nyumba yake hiyo anarudishiwa.

Chanzo: bongo5.com