Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muumini akinukisha, ataka arudishiwe fedha zake za fungu la 10 alizotoa

Fungu La 10 Ataka arudishiwe fedha za fungu la 10 alizotoa

Mon, 13 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja kutoka nchini Nigeria, amelitaka kanisa lake kumrudishia pesa zote alizotoa kama fungu la kumi kwa miaka mingi akidai hana hamu tena ya kuingia mbinguni.

Kufuatia video yake mitandaoni mwanaume huyo ambaye alikuwa akiabudu kwenye kanisa la Dunamis International Gospel Centre, lililopo nchini humo,  amesema kuwa kwa miaka mingi, mchungaji wake amekuwa akitumia kitabu cha Mathayo 6:19 kumshawishi kuwekeza katika ufalme wa Mungu.

Mwanaume huyo anadai kwamba amekuwa muumini wa kanisa hilo tangu mwaka 2013, abapo alitoa kitabu chake cha zaka kama thibitisho kwamba amekuwa akilipa kwa miaka mingi. 

Mwanaume huyo ameongeza kuwa kutokana na hali ya ukata inayomkabili, amesema hataki njaa imtafune hapa duniani na kusisitiza kanisa hilo limrudishie zaka zake ili pia aweze kuwalipa wafanyakazi wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live