Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mufti wa Tanzania azungumzia mafanikio ziara yake Saudi Arabia

56976 Pic+muft

Tue, 14 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi amesema ziara yake ya wiki moja nchini Saudi Arabia ilikuwa na mafanikiomakubwa na imeweza kuitangaza Tanzania kwa viongozi wa kiislamu nchini humo.

Katika ziara hiyo aliyoifanya Mei 3 hadi 10, Sheikh Zuberi  alipata nafasi ya kukutana na viongozi mbalimbali wa Kiislamu nchini humo akiwamo Waziri wa Mambo ya Kiislamu, Abdulratwif Al-Sheikh, Mufti wa Saudia, Abdulaziz bin Abdallah na Imamu Mkuu wa Msikiti wa Macca, Abdulrahman Sudais.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Mei 12 jijini Dar es Salaam, Mufti Zuberi amesema lengo la ziara yake Lilikuwa ni kujifunza jinsi wenzao wa Saudia wanavyoendesha shughuli zao katika kuwahudumia Waislamu.

"Ziara yangu imeitangaza Tanzania kimataifa hasa katika suala la kidini. Nina imani huko mbele itafungua milango mingine ya manufaa," amesema Sheikh Zuberi

Amesema akiwa huko alipata nafasi ya kutembelea Benki ya IDB na kuwaeleza kwamba Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) ina miradi mbalimbali hapa nchini ambayo wanaweza kuifadhili ili kutoa huduma kwa wananchi.

Ametoa wito kwa waislamu nchini kuacha ugomvi na migogoro ambayo haina tija, badala yake wafanye mambo ya maendeleo ambayo yatabadilisha hali walizo nazo sasa na kuwa na hali bora zaidi.

Pia Soma

"Naomba Waislamu watoke kwenye usingizi huo waje kwenye masuala ya maendeleo," amesema kiongozi huyo wa waislamu nchini.

Chanzo: mwananchi.co.tz