Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mufti wa Tanzania aomba darubini ya kutazama mwezi

Operanews1682180589012 Mufti wa Tanzania aomba darubini ya kutazama mwezi

Sat, 22 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amewaomba Viongozi wa Serikali na Wadau kusaidia upatikanaji wa darubini ya kukusanya taarifa za mwandamo wa mwezi ili kumarisha uhakika wa taarifa.

Sheikh Zubeir amesema hayo leo Aprili 22, 2023 katika swala ya Eid El- Fit iliyofanyika kitaifa katika msikiti wa Mfalme Mohamed VI uliopo Wilaya ya Kinondoni ambapo miongoni mwa waliohudhuria swala hiyo ni Rais Samia pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

“Tuna Mabalozi hapa tuna Mawaziri mbalimbali na Wadau wengine, kuna chombo tunakihitaji cha kutazamia mwezi, wenzetu Zanzibar wanacho, wenzetu Kenya wanavyo vingi tunaomba na sisi wale wanaoweza kutushika mkono watusaidie na sisi” 

Chanzo: www.tanzaniaweb.live