Korogwe. Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir ameipongeza Serikali kwa hatua ilizozichukua dhidi ya Daniel Maleki anayedaiwa kuchana kitabu cha dini.
Jana Ijumaa Februari 7, 2020 picha za video zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zilimuonyesha Maleki ambaye ni ofisa biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro akichana kitabu hicho.
Muda mfupi baada ya kusambaa kwa video hizo, alikamatwa na polisi na kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kilosa ambako alisomewa mashtaka na kupelekwa mahabusu baada ya polisi kuwasilisha ombi la kutaka asipewe dhamana.
Mufti ameeleza hayo leo Jumamosi Februari 8, 2020 katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo.
Amesema kuchanwa kwa kitabu hicho hadharani ni kuwachokoza Waislamu na kuvuruga amani na utulivu wa Watanzania.
“Ninaishukuru Serikali kwa hatua iliyochukua dhidi ya kijana huyu, nawaomba Waislamu kuwa watulivu, wasubiri hatua zaidi
Habari zinazohusiana na hii
- Polisi wapinga aliyechana kitabu cha dini kupewa dhamana, apelekwa mahabusu
- Aliyekanyaga kitabu cha dini aingia matatizoni serikalini
Kabla mtumishi huyo hajakamatwa wala kufikishwa mahakamani, Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo baada ya kuona video hiyo aliitisha mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma na kumuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kumsimamisha kazi mtumishi huyo.