Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mufti amteua Ngeruko kuwa Naibu Kadhi Mkuu

MUFTI MKUU Mufti amteua Ngeruko kuwa Naibu Kadhi Mkuu

Thu, 13 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mufti na Shehe Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir bin Ally amemteua Shehe Ally Khamisi Ngeruko kuwa Naibu Kadhi Mkuu wa Tanzania.

Taarifa ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) kwa umma imeeleza kuwa pia Mufti amemteua Mhasibu Mkuu wa Bakwata, Mwenda Said Mwenda kuwa Kaimu Naibu Katibu Mkuu Utawala na Fedha.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Taifa Bakwata na Msemaji wa Mufti, Shehe Khamis Mataka, Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Nuhu Jabir Mruma amemteua Twahir Al-musawaa kuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje Bakwata makao makuu.

Mruma pia amemteua Shehe Othman Ali Kaporo kuwa Mkurugenzi wa Kurani na mambo ya dini Bakwata makao makuu.

Mataka ameeleza kuwa pia Mruma amemteua Tabu Kawambwa kuwa Mkurugenzi wa Habari, Uhusiano na Usalama wa Ndani Bakwata makao makuu. Taarifa imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza Aprili 10, mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live