Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mufti ahimiza upendo akipokea tende tani 50 kutoka Saudi Arabia

11147 Tende+pic TanzaniaWeb

Tue, 10 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar bin Zubeir amewataka wananchi kudumisha upendo miongoni mwao na mataifa mengine ili kuendeleza udugu.

Mufti ametoa kauli hiyo leo Jumanne Julai 10, 2018, wakati wa kupokea msaada wa tende kutoka ubalozi wa Saudi Arabia katika ofisi za Bakwata jijini Dar es Salaam.

Amesema msaada huo ni muendelezo kwa nchi hiyo kuisaidia Tanzania ambapo amesema amepokea boksi 250 sawa na tani 50.

"Msaada huu ulikuwa kwa ajili ya mwezi wa Ramadhani lakini kutokana na changamoto mbalimbali hazikuweza kufika kwa wakati," amesema.

Mufti ameongeza kuwa kwa sasa taratibu za mgao zinaendelea ili kuhakikisha waislamu wanapata tende hizo.

"Tunaishukuru Saudi Arabia kwa msaada huu, hii inadhihirisha jinsi gani wenzetu wana upendo na mahaba kwetu na sisi tudumishe upendo huu," amesema.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo mwakilishi wa Balozi wa Saudi Arabia, Ahmed Al-Ghamdi amesema wataendelea kuisaidia Tanzania katika masuala mbalimbali.

"Si jambo geni kwetu kutoa msaada na tunafanya hivi kwa ajili ya upendo na mahusiano mazuri yaliyopo baina yetu," amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz