Tanga. Mufti wa Tanzania, Abubakar Zubeir ameongoza maelfu ya waumini wa dini ya Kiislamu waliojitokeza kuswali swala ya Eid el Fitr iliyoswaliwa Kitaifa katika msikitini Mkuu wa Ijumaa jijini Tanga.
Swala hiyo imeswalishwa leo Jumatano Juni 5, 2019 na Sheikh Ramadhani Mbarouk na hotuba ya Eid imetolewa na Sheikh Twahir Muhammad Al Musawa
Naibu Kadhi, Muhidin Mgoyogole amewataka Waislamu nchini kuendeleza mema waliyokuwa wakiyatenda wakati wa mwezi wa Ramadhani kwa kuwa ndivyo Uislamu unavyotaka.
Kuhusu mavazi amewaasa Waislamu hususani wanawake kuvaa nguo zenye kulinda maadili ya Uislamu ili kulinda maadili ya Uislamu.
Swala hiyo imehudhuriwa pia na Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, January Makamba, Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, Mbunge wa Tanga Mjini (CUF), Mussa Mbarouk na viongozi mbalimbali wa Serikali na siasa.
Wakizungumza kuhusu nasaha zilizotolewa na Naibu Kadhi waumini waliozungumza na Mwananchi kuhusiana na mavazi wamesema ni kweli wakati wa Ramadhani waumini walionekana kujisiri na miji ilitulia lakini kuanza leo vurugu zitaanza
Pia Soma
- Beki wa Real Madrid atua Tanzania, atembelea Hifadhi ya Serengeti
- Sheikh awataka Waislamu kuyaendeleza mema ya Ramadhan
- Magufuli atoa maagizo kwa Ma-DAS, ofisa tarafa nchi nzima