Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mufti Tanzania aonya masheikh, maimamu wanaotoa mawaidha yasiyofaa

Mufti Tanzania aonya masheikh, maimamu wanaotoa mawaidha yasiyofaa

Mon, 30 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir amesema hivi sasa kuna mmomonyoko wa maadili ya lugha katika mfumo wa utoaji wa mawaidha sehemu mbalimbali zikiwamo za mihadhara.

Amesema mawaidha yanayotolewa hayana lugha ya staha na  hayapo katika mfumo unaotakiwa katika maelekezo ya Mtume Muhammad (S.W).

Sheikh Zubeir ametoa kauli leo Jumamosi Desemba 28,2019 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam kuhusu mwenendo wa utoaji wa mawaidha unaofanywa na masheikh, maimamu na walimu wa madrasa.

Amesema mawaidha yanayotakiwa kutolewa kwenda kwa waumini ni yale yenye staha kwa anayesikiliza sambamba na kumvutia asiyekua Mwislamu kujiunga na dini hiyo.

"Mfumo wa sasa wa mawaidha hasa kwa kina mama ni kutaja maumbile na viungo vyao na mambo wanayoyafanya. Vitu kama hivi vinaondosha na taswira nzuri ya Uislamu, nawaomba masheikh na maimamu waangalie lugha wanazozitumia.”

"Watumie lugha ambazo haziwagusi moja kwa moja kina mama na kuwadhalilisha na kuwafanya  wanaonekana wananyanyasika wakati wanahitaji la kupata mawaidha. Tumeona baadhi yao wakisimama kuzungumza wanaongea mambo ambayo yanaleta matatizo hasa kwa kina mama," amesema Sheikh Zubeir.

Hata hivyo, Sheikh Zubeir amesema anatambua mchango mkubwa na kazi wanayoifanya masheikh na maimamu na watu mbalimbali wanaotoa mawaidha, lakini amewataka kuzingatia  misingi ya lugha katika mchakato huo.

Sheikh Zubeir amewasisitizia masheikh, maimamu na watoaji wa mihadhara  na kuangalia njia sahihi ya utoaji wa mawaidha kwa kuangalia misingi ya lugha yenye staha ili kuwaweka waumini katika mazingira mazuri.

Chanzo: mwananchi.co.tz