Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mufti: Heshimuni viongozi wa dini na serikali

37f2aae88b9e1bb0af2ef28f6a0652be Mufti: Heshimuni viongozi wa dini na serikali

Tue, 19 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SHEIKH Abubakar Zuberi Bin Ally, Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania amekemea tabia ya baadhi ya watu kutoheshimu viongozi wa dini na serikali kwani kufanya hivyo ni kukosa maadili.

“Unakuta watu wanawatolea maneno mabaya viongozi wa dini na serikali, wala hawaogopi, hii ni kukosa maadii, tuendelee kuwaheshimu viongozi wetu na kuwatii,” amesema

Aidha amekemea tabia ya baadhi ya watu wanaopotosha kuwa chanjo ya Corona ni mbaya.

“Wapo wanapotosha kuwa chanjo haifai, katika uislam tunaangalia vitu viwili, kimoja bora na kingine sio bora, kinachotakiwa kufuatwa ni kilicho bora, kuchanja ni jambo jema, hivyo ndugu zangu Waislam ambao hamjachanja mkachanje,” amesema.

Pia alisema bado kuna kesi ambazo hazijamalizwa magerezani na kuiomba serikali izimalize.

Chanzo: www.habarileo.co.tz