Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtume Mwamposa avunja ukimya kuitwa Freemason

Mwamposa Kej.jpeg Nabii Mwamposa

Sun, 12 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa Kanisa la Arise and Shine (Inuka Uangaze) lililopo Kawe jijini Dar es Salaam, Mtume na Nabii Boniface Mwamposa amesema anawashangaa watu wanaomuita yeye ni freemason kutokana na staili yake ya maisha.

Mwamposa ambaye amekuwa maarufu katika huduma yake ya uchungaji hasa kwa kutumia mafuta ya upako, amesema hayo leo Jumapili, Februari 12, 2023 wakati akizungumza na waumini wake kanisani kwake.

Aidha, Mwamposa amedai baadhi ya watu wamekuwa wakihoji maamuzi yake ya kubadili Viatu anapokuwa Kanisani akidai anafanya hivyo kwa kuwa kuna Viatu ambavyo vikimwagikiwa na Mafuta vinaharibika.

"Kila kitu nikifanya inakuwa gumzo, juzi nilikuwa Bungeni, nilifanya ibada kwa Wabunge, nilipotoka pale nashangaa picha zinazagaa kuhusu mimi kwa mabaya licha ya kuwa watumishi tulikuwa wengi.

Mwamposa amesema: "Yaani mimi nianze kujibizana na watu kwenye mitandao wanavyosema Mwamposa Freemason, nami niingine kwenye mitandao kuanza kuwajibu kuwa mimi si Freemason, sina muda huo hata kidogo.

"Hata nikiwa hapa (Kanisani) huwa wanashangaa ninavyobadilisha viatu, nabadilisha kwa kuwa mafuta ninayotembea nayo yakimwagikia kwenye kiatu yanakiharibu, hivyo nafaa viatu ambavyo nakuwa comfortable kuzunguka nacho.

"Hata wakiona nimevaa cheni inakuwa gumzo, hata nikichukua kitambaa hapa madhabahuni nikafuta jasho naambiwa Mimi ni Freemasons kwanini?" Amehoji Mtume Wenu Mwamposa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live