Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa miaka sita ateketea kwa moto ndani

Mon, 24 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Mtoto mwenye umri wa miaka (6) ameteketea kwa moto baada ya chumba alimokuwa amelala kuungua kwa moto wa mshumaa mtaa wa NHC Mugumu wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara.

Mwenyekiti wa mtaa Elias Nyamraba akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Juni 22,2019 amesema tukio limetokea majira ya saa 9 usiku na aliyefariki ni Kaleb Mwita huku aliyenusurika ni Robert Mwita (8).

Akisimulia tukio hilo, Robert amesema aliwasha mshumaa saa 2 usiku baada ya umeme kukatika na kulala lakini ilipofika majira ya 9 usiku alisikia joto kuangalia akakuta moto unawaka na kumwamsha mdogo wake ili watoke ndani kwenda nje.

Alisema mdogo wake alitoka lakini kabla alilazimika kurudi ndani kuchukua kanda mbili zake ndipo alipofikwa na mauti.

Mkuu wa wilaya hiyo, Nurdin Babu amesema polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Undani wa habari hii kuhusu simulizi ya mtoto Robert alivyotaka kumwokoa mdogo wake na kilichomponza  hadi akafikwa na mauti usikose gazeti la Mwananchi kesho Jumapili Juni 23, 2019

Pia Soma



Chanzo: mwananchi.co.tz