Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moto waacha simanzi soko la Makoroboi jijini Mwanza

95431 Pic+moto Moto waacha simanzi soko la Makoroboi jijini Mwanza

Fri, 14 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Moto uliozuka saa 9 alfajiri leo Jumatano Februari 12, 2020 katika soko la Makoroboi mkoani Mwanza umeacha simanzi kwa wafanyabiashara kutokana na bidhaa zao kuteketea.

Moto huo uliowaka kwa dakika takribani 45  ulizimwa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na wananchi, hakuna bidhaa zilizookolewa.

Siffa Siraji amesema alikuwa anategemea biashara aliyokuwa akiifanya katika eneo hilo kuendesha maisha yake, “kipato nilichokuwa nakipata ndio nilikitumia kuitunza familia yangu. Kwa yaliyotokea sijui nitaihudumia vipi familia yangu.”

Timoth Clemence amesema taarifa za kuzuka kwa moto huo amezipata baada ya kupigiwa simu na kusababisha apate mshtuko bila kujua la kufanya.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana,  Dk Philis Nyimbi amethibitisha amewataka wafanyabiashara kuwa watulivu wakati vyombo vya dola vinaendelea kuchunguza chanzo cha moto huo.

Bidhaa za wafanyabiashara wadogo 159 zimeteketea huku mabanda 65 nayo yakiteketea.

Pia Soma

Advertisement

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Chanzo: mwananchi.co.tz