Unguja. Mkutano wa viongozi wa dini kutoka mataifa mbalimbali utafanyika Zanzibar kuanzia Septemba 21 hadi 23, 2019.
Wakizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Septemba 14, 2019 baadhi ya viongozi hao wamesema mkutano huo unalenga kuleta umoja kwa wananchi wenye imani tofauti.
Mshauri wa waziri wa katiba na sheria Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga amesema unalenga zaidi uhamasishaji wa amani na ushirikiano wa waumini wa dini zote.
Amesema Waislamu wamekuwa wakihubiri upendo na amani, hakuna sababu ya kuchukiwa na waumini wa dini nyingine.
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar, Agustino Shao amesema mkutano huo utafungua fursa mpya za ujenzi wa amani
Pia Soma
- Lyon yashindwa kuipiku PSG kileleni Ufaransa
- Hazard, Suarez warejea uwanjani leo Hispania, Messi bado
- Guardiola: Raheem? Hakuna kama Ronaldo na Messi duniani