Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkurugenzi atuhumiwa kuua kwa risasi

40122 Dedpic Tanzania Web Photo

Tue, 5 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa Itigi, Pius Luhende na askari wawili wa wanyama pori wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua kwa risasi muumini aliyetajwa kwa jina la Isaka Petro akiwa kanisani.

Akizungumza na Mwananchi jana kuhusiana na tukio hilo lililotokea Jumamosi iliyopita, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), Selemani Jafo alisema; “Ni kweli kumetokea mauaji hayo na hadi sasa mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Itigi na askari wawili wa wanyama pori wapo ndani.

“Kwa kuwa nipo barabarani, sijajua undani wa jambo lenyewe. Siwezi kuzungumza mengi, ila kwa kiufupi ni jambo baya sana lililowahi kutokea, nitatoa kauli baada ya kupata undani wa tukio lenyewe,” alisema Jafo.

Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, mkuu wa Mkoa wa Singida, Rehema Nchimbi alisema suala la mauaji si la kisiasa wala kiutendaji, hivyo linapaswa kujibiwa na Polisi, “Mtafuteni kamanda wa polisi Mkoa wa Singida anaweza kuwa kwenye nafasi nzuri ya kulizungumzia.”

Alipotafutwa, kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida simu yake iliita bila kupokewa.

Mchungaji wa Kanisa la Adventista Sabato yalikotokea mauaji hayo, Manyigina Manyigina alisema alipata taarifa hizo akiwa Manyoni alikokuwa akiendesha ibada nyingine na alilazimika kukatisha ibada na kurejea Itigi ili kujua kilichosababisha tukio hilo.

Alisema alisimuliwa lilivyokuwa na waumini ambao walidai kabla ya mauaji hayo, kulitokea vurugu kanisani hapo wakati wa mafundisho ya sabato saa saba mchana.

“Waumini walinieleza kuwa baada ya kupata chakula cha mchana kanisani hapo, wengine walikuwa wameingia ndani na wengine walikuwa nje, ndipo waliona gari mbili aina ya Land Cruiser za Serikali zikiingia eneo hilo na mkurugenzi alishuka na maaskari watatu.

“Nje walimkuta mzee mmoja wakampiga kisha wakaingia kanisani na kumkaba shati muumini mmoja kabla ya kumkata ngwala na walikuwa wakiulizana ni huyu... hapana siyo huyu wanaulizana na kujibizana wao kwa wao, kisha ofisa mtendaji waliyeongozana (hakumtaja jina) naye akawaambia watoke nje,” alisema. Alidai kuwa walipotoka nje, waliwafungia waumini mlango kwa nje na baada ya muda walirudi na kumpiga risasi muumini mmoja ambaye alifariki dunia papo hapo.

“Najiuliza kwa nini wamekuja kufanya fujo kanisani tena siku ya sabato na kuua, inashangaza sana,” alisema.



Chanzo: mwananchi.co.tz