Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkazi Mirerani aomba wizara imsaidie arejeshewe mgodi wake

20288 Pic+mkazi TanzaniaWeb

Tue, 2 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Mkazi wa Mirerani, mkoani Manyara, Anton Mwiru(65), ameiomba Wizara ya Madini, kumsaidia kurejeshewa leseni ya mgodi wake ambayo inashikiliwa na mfadhili aliyeomba kuendesha mgodi huo na kushindwa kuendesha kwa miaka sita sasa.

Akizungumza na Mwananchi, leo Oktoba 1, 2018 Mwiru amesema mwaka 2002, yeye na mmiliki mwenza wa mgodi wenye namba PML 000344NZ uliopo eneo la Kitalu D, Tausi Faraji, waliingia makubaliano na mfadhili, Kilempu Kinoka kuchimba madini  mwaka 2002 lakini hadi sasa ameshindwa kuchimba.

"Tangu tumekubaliana afadhili kuchimba mwaka 2002, hajachimba na ameendelea kushikilia leseni yetu baada ya kuongeza jina lake kwenye leseni, ingawa sisi tumekuwa tukilipa ada kila mwaka" amesema.

Amesema kutoendelezwa kwa mgodi huo, kunawafanya kuishi katika maisha magumu na familia zao kwani, licha ya kupata wafadhili, wengine wameshindwa kuanza kuchimba kwa kuwa leseni inashikiliwa na mfadhili huyo.

"Suala hili tayari tulilifikisha ofisi ya madini Kanda ya Kaskazini na alikiri kushindwa kuendeleza mgodi lakini amegoma kusaini barua ya kujitoa kwenye leseni ya mgodi akidai malipo jambo ambalo si sahihi," amesema.

Kinoka ambaye pia ni diwani wa kata ya Naisinyai, Mirerani, alipotakiwa kuelezea mgogoro huo, amesema tayari amejitoa katika mgodi huo na sasa hajihusishi na uchimbaji wa madini ya Tanzanite.

"Mimi nimewarudishia mgodi wao, sasa nashangaa huyu mzee anaendelea kunifatafata ili anichafue, lakini kwa sasa sitaki kulizungumza suala lake," amesema.

Awali, mgogoro huo, tayari ulifikishwa kwa aliyekuwa kamishna msaidizi wa madini Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Joel Mchwampaka ambaye aliagiza kumalizwa mgogoro kwa wamiliki kubaki na mgodi wao lakini bado uamuzi huo haujatekelezwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz