Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miili ya Askofu Timanywa, mtawa yaagwa Mwanza

14606 Miili+pic TanzaniaWeb

Thu, 30 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Mwili wa mtawa Suzan Bathlomeo (48) aliyefariki juzi huku ikidaiwa alijirusha kutoka ghorofani katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando mjini hapa umesafirishwa kwenda Bukoba, Kagera kwa ajili ya maziko.

Akizungumza na gazeti hili jana, ofisa uhusiano wa Hospitali ya Rufaa Bugando, Lucy Mogela alisema misa hiyo ilifanyika katika Kanisa Katoliki Bugando kabla ya kuanza safari.

Kuhusu taratibu za mazishi na taarifa nyingine muhimu, Lucy alisema zitatolewa na msemaji wa shirika la watawa la Mtakatifu Theresia lililopo mjini Bukoba.

Hata hivyo, kamanda wa polisi mkoani hapa, Jonathan Shanna alisema juzi kuwa uchunguzi umebaini ofisi aliyokuwa akifanyia kazi mtawa huyo kuna tuhuma za upotevu wa zaidi ya Sh300 milioni zilizosababisha watumishi wenzake wanane kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi na baadhi kufukuzwa.

Wakati huohuo, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, Yuda Thadeus aliongoza misa ambapo mwili wa Askofu mstaafu wa Jimbo la Katoliki Bukoba, Nestor Timanywa (81) kwenye Kanisa Kuu la Epifania Parokia ya Bugando, jijini Mwanza. Mwili huo unatarajiwa kusafirishwa leo kwenda mjini Bukoba kwa maziko.

Katika misa hiyo iliyofanyika jana jioni, Askofu Thadeus alisema Timanywa alihudumia Jimbo la Bukoba kama Askofu Mkuu kwa miaka 39 na kustaafu 2013.

Akitoa ushuhuda, Padri Deodatus Rwehumbiza aliyemwakilisha Askofu wa Jimbo Katoliki Bukoba, Desderius Rwoma alisema Timanywa amefariki kwa ugonjwa wa saratani. “Saratani hiyo ilikuwa inazunguka kutoka kiungo kimoja mpaka kingine na polepole ikawa inamdhoofisha mpaka jana (Agosti 28) alipoaga dunia,” alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz