Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mhubiri: Ukitaka miujiza usifanye ngono

Mhubiri Wakarura .jpeg Mhubiri Wakarura Nyutu

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mhubiri maarufu nchini Kenya, Wakarura Nyutu ametoa ushauri kwa vijana ambao wanataka miujiza kufanyika maishani mwao.

Nyutu amesema maombi hayataki mambo ya uzinzi na uasherati kwani huwa ni kizuizi cha maombi kwa Mungu na majibu yao kuchelewa.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, amewashauri wale ambao wanapanga kufanya maombi kwa ajili ya jambo fulani kuacha mambo ya kufanya uzinzi na uasherati.

"Wakati unaomba ili uweze kupata kitu muhimu, usijihusishe na suala la ngono kipindi hicho haswa iwapo uko singo. Kufanya mapenzi huzuia miujiza kufanyika," alisema Wakarura.

Mhubiri Wakarura anasema ni kosa kushiriki kitendo cha uzinzi na uasherati wakati upo kwenye maombi na unataka muujuzi kwa kufanya hivyo huwa inazuia majibu ya maombi yetu kutokea na muujiza kufanyika.

Amewataka wanaotafuta nguvu za Mungu na miujiza wajinyime kitendo cha mapenzi ili Mungu aweze kusikia maombi yao na kuyatimiza kwa wakati.

Mhubiri Wakarura hujulikana kwa injili yake ambayo huwalenga vijana akisema furaha yake ni kuokoa mioyo ya wengi duniani kote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live