Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji wa Wasabato aikumbusha jamii kuhusu wenye uhitaji

52137 Pic+wasabato

Mon, 15 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waumini wa Kanisa la Wadventista Wasabato Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam wametakiwa kuwa na mfumo wa kila siku wa kuwaona watu wenye uhitaji na wasisubiri siku ya tukio ndiyo wawakumbuke.

Hayo yamesemwa na mchungaji wa kanisa hilo, Baraka Butoke leo Jumamosi Aprili 13, 2019 alipokuwa kwenye ibada ambayo leo ni 'Siku ya  ujirani mwema' ambapo wamewaalika watoto wanaoishi katika mazingira magumu na waathirika wa dawa za kulevya.

Mchungaji Butoke amesema waumini wa kanisa hilo wawe na upendo kwa wahitaji hao na isiwe siku moja au mbili kwa mwaka badala yake iwe ni mfumo wa maisha yao.

Amesema watoto wanaoishi katika mazingira magumu na walioathirika na dawa za kulevya wanajiona hawana thamani katika jamii inayowazunguka hivyo kanisa hilo linawaona na kuwathamini.

"Katika maisha haya unaweza ukapitia changamoto ambayo ikakupelekea kufanya dhambi hivyo haijalishi upo kwa namna gani Mungu atakusaidia kutoka hapo ulipo na kuwa mtu mwingine," amesema Mchungaji Butoke.

Amesema katika dunia hii watu wanaweza kukudharau na hali unayopitia hivyo kanisa hilo linawapokea na kuwathamini na kuwafikiria wale waliokata tamaa.

Mwenyekiti wa Wazee wa Jumuiya ya Waislamu, Amiri Abeid amesema watu wasikilize mafundisho yanayotolewa na viongozi wao wa dini na wayatekeleze ili nchi iweze  kuwa ya amani.

Amesema lengo ni kuhakikisha Mungu anaabudiwa hivyo matatizo yote yanatoweka hata Serikali inakuwa haina shida ya kuendesha nchi.

Kiongozi wa Soba ya Kigamboni, Adam Lupatu ameiomba jamii kupunguza ukali wa mtazamo wanavyolichukulia tatizo la waathirika wa dawa za kulevya kwani inaweza ikatokea ndugu wa karibu kuwa na tatizo hilo.



Chanzo: mwananchi.co.tz