Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji azichambua wizara mbele ya Rais Magufuli

Wed, 4 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mchungaji wa Kanisa la Baptist Tanzania, Daniel Mgogo amemwomba Rais John Magufuli kuzisimamia wizara zake  ili ziweze kufanya kazi kwa ushirikiano na kuepusha watu kubomolewa nyumba zao kutokana kujenga katika maeneo yasiyostahili.

Ameyasema hayo leo Jumatano Septemba 4, 2019 katika mkutano wa mashauriano baina ya Rais Magufuli na watumishi wa Bodi ya usajili wa Makandarasi (CRB), Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) ambao unafanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema wananchi wamekuwa wakiumizwa na vitendo vya kubomolewa nyumba zao ili kupisha ujenzi wa barabara jambo ambalo lingeweza kuzuilika endapo wizara zingeshirikiana.

“Mtu amejenga katika eneo la barabara, anaomba umeme anawekewa umeme, anaomba maji anawekewa, leo tena unakuja unaniambia ulikosea na inabomolewa, hii inaonyesha kuwa kama vitu vikifanyika kwa utaratibu mzuri itawasaidia wananchi,” amesema Mchungaji huyo huku akishangiliwa na wataalamu hao wa ujenzi

Amesema wakati mwingine wananchi wamekuwa wakiingia katika ugomvi na Serikali kwa sababu wataalamu wa ujenzi wamekuwa hawawasaidii, jambo ambalo limekuwa likiwafanya baadhi kuhisi kama wanaonewa.

“Tusaidieni kusema uwanja huu haupo sehemu sahihi tusaidieni nyie wakandarasi, tusaidieni nyie wahandisi sisi kutoka vijijini ndiyo tunabomolewa nyumba hawa watoto wa mjini ni wajanja wanajua hili ni eneo la barabara,” amesema

Pia Soma

Advertisement

 “Mheshimiwa Rais (John Magufuli) kuna watu umekosana nao siyo wewe, wanasema umevunja nyumba zao lakini kiukweli siyo wewe waliofanya ni miongoni mwa hawa waliopo kwa sababu tulipopata viwanja tulijenga na wakatuwekea umeme na maji na baadaye wakatuambia tumejenga sehemu isiyokuwa yenyewe,” amesema Mgogo huku Rais Magufuli naye akionekana kufurahia.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz