Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji atoa mpya kuhusu vijana wazinzi

33531 Pic+uzinzi Tanzania Web Photo

Wed, 26 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Pwani. Mchungaji wa Kanisa Anglikana Tumbi Kibaha mkoani Pwani, Exavia Mpambichile amesema atafanya maombi ili vijana wanaozini  katika nyumba za wageni kutoka wakiwa wamenaswa na magodoro mwilini ili wasirudie kutenda dhambi hiyo.

Ametoa kauli hiyo jana Jumanne Desemba 25, 2018 katika mahubiri ya ibada ya Krismasi, akibainisha kuwa kama hali hiyo itatokea itakuwa fundisho kwa vijana wote wanaofanya uovu huo.

"Kama kuna vijana watakwenda nyumba za wageni kwa ajili ya kufanya matendo yasiyofaa, nitafanya maombi ili lile godoro watakalolalia linasie kwenye mwili na akitoka atembee nalo mtaani ili siku nyingine asifanye hivyo,” amesema.

Amesema waumini wa kanisa hilo wanaposherehekea Sikukuu ya Krismasi wanapaswa kujihadhari na mambo yasiyofaa, badala yake wajikite kudumisha upendo, ushirikiano na kufanya mambo mema.



Chanzo: mwananchi.co.tz