Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji ataka wanawake wagombee Serikali za mitaa

53601 Pic+mchungaji

Tue, 23 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati uchaguzi wa Serikali za mitaa ukikaribia, wanawake wametakiwa kujitokeza kugombea nafasi hizo kwa sababu wanao uwezo.

Akihubiri katika ibada ya Jumatatu ya Pasaka Mchungaji Lazaro Samweli wa kanisa la Shekemu Trust la Pugu jijini Dar es Salaam amesema watu wa kwanza kutoa habari za kufufuka kwa Yesu ni wanawake.

Amesema kwamba kama wanawake walikuwa wa kwanza kueneza habari hizo wanaweza kugombea nafasi za uongozi na wakawa mfano wa kuigwa.

"Mkigombea mnaweza kuja kusaidia jamii yenu kwa sababu watoto, wanawake wenzenu hata wanaume wanahitaji mchango wenu, kama una sifa ya kuwania usisite, jitokeze na uchukue fomu," alisisitiza na kuongeza: "Ni wakati wenu kwenda kwenye kinyang'anyiro hicho."

Mchungaji huyo ambaye alitumia muda mwingi kuombea amani ya nchi hasa wakati ya uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, amesema wanawake ni walezi wazuri hivyo wakiinuka kugombea wenye uwezo wapewe nafasi.

Alimpongea Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuonyesha mfano wa uongozi wa ngazi ya juu katika taifa ikiwa ni mara ya kwanza kwa historia ya nchi kuwa na kiongozi wa nafasi hiyo mwanamke.

"Yesu alipofufuka tu alisema amani iwe kwenu hivyo nami niombee amani kwa taifa letu, viongozi wote na Watanzania," amesisita mchungaji huyo.



Chanzo: mwananchi.co.tz