Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji ampoza dereva wa RC Mara

70351 Pic+ajali

Wed, 7 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Musoma. Mchungaji wa Kanisa la Zion Gospel Assembly, Eliya Amas amemtaka dereva wa Mkuu wa mkoa wa Mara, Shida Masaba kuwa pamoja na familia yake na kumuachia Mungu mambo yote yaliyotokea.

Amas ametoa kauli hiyo leo Jumatano Agosti 7, 2019 katika ibada ya mazishi ya Kasobi Shida, mtoto wa Masaba aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Jumatatu Agosti 5, 2019 katika Hospitali ya Mkoa wa Mara.

Kasobi alifikishwa katika hospitali hiyo baada ya kupata ajali Jumamosi Agosti 4, 2019 wakati akiendesha gari la mkuu wa mkoa huo, Adam Malima ambalo huendeshwa na baba yake.

Mchungaji huyo amesema kuna tabia za watu kuhusisha matukio ya namna hiyo na ushirikina, wapo watakaoanza kumsaka nani mbaya badala ya kumuachia Mungu kila jambo.

Ametaka msiba huo kuwa funzo la upendo katika familia, akisisitiza kuwa kila binadamu ni lazima afe.

"Shida nakuomba uishike na kuibeba familia yako, usikubali jambo hili kuwa chanzo cha mfarakano katika familia yako badala yake litumike kama kitu cha kuimarisha upendo,” amesema mchungaji huyo.

Habari zinazohusiana na hii

Chanzo: mwananchi.co.tz