Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji akumbusha maombi kukabili magonjwa

377a3cb2ebd636e6b45448274f2ca9b9 Mchungaji akumbusha maombi kukabili magonjwa

Wed, 17 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MKURUGENZI wa Uinjilisti na Elimu, kanisa la EAGT, Kanda ya Kati Mchungaji Nason Msanjila amesema pamoja na wataalamu wa afya na viongozi wa serikali kuwahamasisha watanzania kujikinga na maambukizi nyumonia kali bado kuna kila sababu ya kumtanguliza Mungu kwa maombi ili kuepusha balaa hilo.

Mchungaji Msanjila amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa ibada iliyofanyika katika kanisa hilo lililopo Uzunguni jijini Dodoma.

Alisema kuwa pamoja na elimu inayotolewa toka kwa wataalamu na viongozi mbalimbali wa serikali juu ya kujilinda na maambukizi hayo ya covidi – 19 bado kuna ulazima mkubwa wa kumtegemea Mungu kwa maombi.

“Pamoja na tunamtegemea Mungu kwa kila jambo,lakini pia tuzingatie maelekezo ya wataalamu na viongozi wetu wa serikali ambao wamekuwa wakihimiza na kutoa elimu muda wote kwa ajili ya kujiepusha na maambukizi hayo”alisema.

Aidha ameshauri Watanzania kuhakikisha wanajishughulisha na shughuli mbalimbali za uzalishaji ili waweze kujipatia kipato,badala ya kukaa majumbani kwa kuhofia kuambukizwa homa hiyo ya mapafu.

Alisema ili watanzania waimarike kiuchumi ni lazima kujikita kwenye kufanya kazi za uzalishaji,badala ya kukaa majumbani kwa kuwa kuna uwezekano pia wa kujikuta na umasikini ambao unaoweza kusababisha kushindwa hata na kujilinda kwenye maisha ya kila siku.

Chanzo: habarileo.co.tz