Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji aibuka, aitaka Sh1 bilioni ya ‘Mo’ Dewji

Mon, 22 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Mchungaji wa Mitume, Manabii na Maaskofu Tanzania wa Kanisa la Emmaus Bible Church Pentecostal lililopo Mbezi Kibanda cha Mkaa jijini Dar es Salaam, Komando Mashimo amesema Sh1 bilioni iliyotangazwa na familia ya mfanyabiashara maarufu, Mohammed Dewji ‘Mo’ ni ya kwake.

Familia ya ‘Mo’ Dewji ilitangaza dau hilo nono baada ya bilionea huyo kutekwa na watu wasiojulikana Oktoba 11, alfajiri katika hoteli ya Colosseum Oystarbay jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.

Mashimbo amesema hayo leo Jumapili Oktoba 21, 2018 kanisani kwake wakati wa ibada ya kumshukuru Mungu baada ya  kupatikana kwa ‘Mo’ mwaka huu siku ambayo aliitabiri mchungaji huyo kuwa atapatikana. 

"Baada ya ‘Mo’ Dewji kupatikana, nilipokea simu nyingi sana lakini moja ya simu iliniuliza kwa hiyo mchungaji bilioni moja ni yako? Nilicheka sana," amesema.

Amesema baada ya baba mzazi wa ‘Mo’ Gullam Hussein Dewji kutangaza dau na kuweka namba zake nilimpigia Gullam nikamweleza awe na imani mwanaye atapatikana Oktoba 20, 2018.

"Naweza kusema hiyo bilioni moja ni yangu kama ataamua kutoa maana nimetabiri ataonekana na ameonekana, kweli na ikitokea amekubali kunipa hiyo pesa mimi nitamuomba tu anijengee kanisa," amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz