Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji Kimario achangisha 425

Mchungaji Kimario Achangisha 425 Mchungaji Kimario achangisha 425

Mon, 24 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchungaji Dr. Eliona Kimaro wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama, Jumapili ya jana April 23 2023 katika Usharika wa Kondeni Matala uliopo Himo Mkoani Kilimanjaro, amefanikisha zoezi la kuchangisha jumla ya shilingi milioni 425 za umaliziaji wa ujenzi wa Kanisa hilo na kuvuka lengo la milioni 400 zilizokuwa zikihitajika awali.

Katika harambee hiyo jumla ya ahadi na pesa taslimu ni shilingi milioni mia nne ishirini na tano (425) huku pesa taslimu zilizotolewa papohapo zikiwa ni shilingi milioni sabini na nane (78)

Miongoni mwa walioshiriki Ibada hiyo na kuchangia ni pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba aliyetoa milioni 25 yeye pamoja na Marafiki zake, Naibu Waziri wa Afya Dr. Godwin Mollel, Wabunge Easter Bulaya na Halima Mdee waliotoa milioni 9, Priscus Tarimo wa Moshi Mjini, Mbunge wa Vunjo Dr. Charles Kimei, Mbunge wa Same Magharibi Dr. Mathayo David Mathayo, Mbunge Silvestry Fransis Koka wa Kibaha na Mbunge wa Makete Festo Sanga.

Zoezi hilo lilifanikishwa na Watu mbalimbali wakiwemo Marafiki wa Dr. Kimaro waliosafiri kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo Zimbambwe, Marekani, Sudan na Mikoa ya Tanzania kama Dar es salaam, Dodoma na Arusha kuja kuhudhuria ibada ya shukrani ya Mchungaji huyo katika Usharika wake huu wa nyumbani anakotokea na ndiko alikopatia huduma zake za kiroho toka akiwa Mdogo ikiwemo kubatizwa.

Ibada iliongozwa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania na Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo ambapo mahubiri yote yatapatikana kwenye youtube ya millardayo baadaye hii leo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live