Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji KKKT ataka Watanzania kujitafakari mienendo yao

89890 KANISANIPIC Mchungaji KKKT ataka Watanzania kujitafakari mienendo yao

Fri, 27 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Mchungaji wa usharika wa Kihonda Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) mkoani Morogoro, Isaya Kairanga amesema sasa ni wakati wa Watanzania kujitafakari kwa mienendo yao katika kipindi cha kusherehekea sikukuu ya Krisimasi.

Kairanga amesema hayo jana usiku Jumanne Desemba 24, 2019 wakati akihubiri ibada ya mkesha wa Krisimasi.

Amesema ni jambo la kushangaza kuona watu wakifanya mikesha katika sehemu za starehe na kusahau kumwabudu Mungu aliyewawezesha kufikia walipo.

Mchungaji huyo amewataka wazazi na walezi nchini Tanzania kutochoka kutoa malezi mema kwa watoto wao hasa kipindi hiki cha utandawazi kwani vijana wengi wameonekana kukengeuka kimaadili.

"Maombi ya kila mara ni muhimu kwa watoto wetu, tusichoke kabisa wapendwa na hii itasaidia kujenga kizazi chema," amesema.

Mchungaji huyo pia ameeleza Kuwa namna watu wasivyopendana na kujengeana uadui hivyo akawataka Watanzania kuacha kufarakana na kujinyeyekeza mbele ya Mungu kwani uso wa Mungu wakati wote umekuwa karibu.

Pia, amesema siku ya kuzaliwa kwa Bwana Yesu Kristo kukawe njia kwa wanadamu kwa kuwakomboa huku akiwataka kufungua mioyo yao na kuwa karibu na mwana wa Mungu.

Katika mahubiri hayo mchungaji Kairanga amewataka wananchi kudumisha amani, upendo na kuwa wavumilivu huku akiwataka kufanya kazi kwa bidii ili kukuza kiuchumi.

Chanzo: mwananchi.co.tz