Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji EAGT ataka chaguzi Tanzania zihamasishe mshikamano

90661 Mchungaji+pic Mchungaji EAGT ataka chaguzi Tanzania zihamasishe mshikamano

Thu, 2 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kiongozi wa Kanisa la la Evangelistic Assemblies Of God Tanzania (EAGT) Sinza, Dar es Salaam Mchungaji Alphonce Mwanjala amewaomba Watanzania kuzitazama chaguzi mbalimbali kama njia ya kuleta mshikamano na umoja wa kitaifa badala ya kuwa chanzo cha chuki na utengano.

Mchungaji Mwanjala amelisema hilo jana Jumatano Januari 01, 2019 katika hafla maalum aliyoiandaa kanisani hapo ikihusisha wachungaji mbalimbali aliowaandaa na kuwalea ikiwa ni sehemu ya sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya 2020.

Akizungumza katika ujumbe kwenye hafla hiyo, Mchungaji Mwanjala alisema elimu ya uchaguzi inapaswa kuingia vyema vichwani mwa Watanzania na viongozi pamoja na vyama ili usigeuke chanzo cha migogoro kama ambavyo imekuwa ikitokea katika miaka ya hivi karibuni.

"Nami ningekuwa tu kama tungalikuwa na nafasi ya kusema ni kwamba Baba wa Taifa hili (Hayati Mwalimu Julius Nyerere) alifanya kazi kubwa ya kutuweka pamoja na tungependa ule umoja uendelee.”

“Mambo yote tulikuwa tunaangalia huko nyuma, ninamsikiliza Baba wa Taifa wakati akitoa hotuba zake, wakati mwingine anakuwa mkali kwa mambo ya mataifa mengine wanapotukandamiza lakini baadaye unakuta tena wamekaa pamoja wanacheka,” alisema.

“Sasa hili jambo kwamba sisi katika uchaguzi sio ugomvi. Ni tabia yetu tuliyoichagua sisi Watanzania kwamba kumpata kiongozi ni lazima tufanye uchaguzi. Na mwenye kuchaguliwa basi huyo ndiyo tukubaliane kuwa aliyechaguliwa na mwenye kushindwa naye ajue kwamba anayo nafasi nyingine,” alisema

Chanzo: mwananchi.co.tz