Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji Anglikana ataka waumini kusameheana madeni ya 2019

90529 Madeni+pic Mchungaji Anglikana ataka waumini kusameheana madeni ya 2019

Thu, 2 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kibaha. Mchungaji wa Kanisa Anglikana Mkoa wa Pwani nchini Tanzania, Exavia Mpambichile amewataka waumini wa kanisa hilo kusamehe madeni ya watu waliowakopesha kwa kipindi cha mwaka 2019 ili kuanza upya na kila kitu mwaka 2020.

Mchungaji Mpambichile aliyasema hayo jana usiku Jumanne Desemba 31, 2019 wakati wa mahubiri ya mkesha wa mwaka mpya wa 2020 uliofanyika kwenye kanisa la Mtakatifu Gabriel Tumbi Kibaha.

Alisema waumini hao kutolipizana visasi miongoni mwao pindi inapotokea wametofautiana kwa namna yoyote na badala yake wasameheane.

"Mnapoanza mwaka mpya wekeni msamaha mbele kwa kusameheana na hata madeni ambayo mlikuwa mnadaiana katika kipindi cha mwaka jana sameaneni ili muanze upya kwa kila kitu,” alisema Mchungaji Mpambichile huku waumini wakishangilia

Pia, aliwataka waumini hao kuendelea kuwaombea mema watu wanaojihusisha na vitendo viovu ili neema ya Mungu iwashukie wabadilike na kuacha kujihusisha na vitendo viovu. 

Aliwataka waumini hao kuiombea Serikali, askari polisi, magereza na Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) pamoja na walimu wa shule za msingi na sekondari ili waendelee kutenda kazi kwa kufuata haki kwa jamii.

Chanzo: mwananchi.co.tz